NEWS

Monday 27 December 2021

Watalii wavutiwa na wanyamapori wakisherehekea Krismasi ndani ya Hifadhi ya Serengeti
MAKUNDI ya watalii kutoka mataifa mbalimbali wamesherehekea Sikukuu ya Krismasi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Jana Desemba 26, 2021, Mara Online News imeshuhudia misururu ya magari yaliyosheheni watalii wa ndani na wa kigeni kutoka mataifa tofauti wakivutiwa kutazama na kupiga picha makundi ya wanyamapori katika maeneo mbalimbali hifadhini hapo.


Watalii wengi walionekana eneo la Seronera, wakivutiwa na uwepo wa wanyamapori wa aina mbalimbali, wakiwemo duma, simba, twiga, nyumbu na pundamilia.

Aidha, kivutio kingine kikubwa kwa watalii hao kilikuwa mni idadi kubwa viboko waliokuwa wamejaa katika mto Seronera.Kwa mujibu wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Masana Mwishawa, idadi ya watalii wa nje na ndani ya nchi wameendelea kuongezeka katika hifadhi hiyo miezi ya hivi karibuni.Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni kivutio kikubwa cha utalii, ambapo imeshinda Tuzo ya Hifadhi Bora Afrika kwa miaka mitatu mfululizo, yaani 2019, 2020 na 2021.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages