NEWS

Monday, 12 January 2026

Serikali yaipongeza Barrick kwa kufunga mgodi wa Buzwagi kwa njia za kitaalamu



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya (katikati), akiwa ziarani katika Kongani ya Buzwagi.

Na Mwandishi Wetu
Kahama
-------------

Serikali imeipongeza kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwa kufunga mgodi wa Buzwagi kwa njia za kitaalamu na kulifanya eneo hilo kuwa kivutio kwa wawekezaji.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya, alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki iliyopita, alipotembelea maeneo mbalimbali ya Kongani ya Buzwagi wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

"Buzwagi ni eneo sahihi kwa uwekezaji na limepangiliwa vizuri na wadau wote wanaolisimamia, ikiwemo kampuni ya Barrick," alisema Naibu Waziri Chaya.

Alisema Kongani ya Buzwagi ya Viwanda itachochea ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Kongani hiyo ina vigezo vyote vya kuwavutia wawekezaji na ina mazingira rafiki ya ufanyaji biashara. Eneo hilo lina ukubwa wa ekari 1,331.

Naibu Waziri Chaya aliwahamasisha Watanzania kuchangamkia uwekezaji katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages