NEWS

Tuesday 4 January 2022

Fahamu shule ya wilayani Tarime iliyofaulisha wanaafunzi wengi kwenda sekondari za vipaji maalumu nchini 2021



ILIYOKUWA Makima English Medium School katika mji mdogo wa Sirari wilayani Tarime, Mara sasa inaitwa Moregas English Medium School.

Moregas English Medium School inamilikiwa na mwekezaji mzawa, Cosmas Mseti ambaye alinunua iliyokuwa Makima English Medium School.

“Tumebadilisha jina la shule ili liendane na mipango yetu, tuna ndoto za kuifanya shule hii kuwa bora kitaifa,” Mkurugenzi huyo wa Moregas English Medium School amesema katika mahojiano maalumu na Mara Online News, leo Januari 4, 2022.

Mkurugenzi Mseti akionesha sehemu ya majengo ya shule hiyo

Shule hiyo iliyopo eneo la Majengo Mapya, Sirari, ni ya bweni na kutwa na kwa sasa ina wanafunzi 612 wa darasa la awali hadi la saba na walimu 20.

Mwaka jana (2021) Moregas English Medium School iliibuka kinara katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, ambapo ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya kwa ufaulu mzuri na kufaulisha watoto wengi kwenda shule mbalimbali za vipaji maalumu nchini.

Mkurugenzi Morega anawakaribisha wazazi na walezi kupeleka watoto wao kupata elimu bora katika shule hiyo yenye majengo ya kisasa, walimu wabobezi, mazingira ya kuvutia na wezeshi ya kujifunza kwa weledi.



Kwa mujibu wa Mseti, kwa sasa Moregas English Medium School ina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000 na itaanza kufundisha masomo ya kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wanafujnzi mwaka huu.


Mseti akionesha jengo la kisasa la TEHAMA shuleni hapo

Mseti anasema ada za masomo katika shule hiyo ni nafuu na rafiki, zinazolipwa kwa awamu, huku huduma za maji, umeme na usafiri zikiwa za uhakika.

Pia, huduma za chakula na malazi kwa wanafunzi wa bweni ni bora na rafiki.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages