NEWS

Monday 3 January 2022

Viongozi wa Chama, Serikali waaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mipango TarimeVIONGOZI mbalimbali wa chama tawala - CCM na Serikali (pichani juu) wameungana na watumishi wengine kuanga mwili wa aliyekuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Frederick Mallya aliyefariki dunia jana Januari 2, 2022 katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

 Mwenyekiti Ngicho akitoa heshima za mwisho

Tukio hilo limefanyika leo Januari 3, 2022 mchana katika viwanja vya ofisi ya zamani ya halmashauri hiyo iliyopo Bomani, kabla ya mwili wa Mallya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Moshi, Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

 DC Mntenjele akitoa heshima za mwisho

Viongozi walioshiriki katika tukio la kuaga mwili wa Mallya ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho na Mkuu wa Wilaya (DC) hiyo, Kanali Michael Mntenjele.

 Viongozi wa Chama na Serikali wakifuatilia jambo wakati wa kuaga mwili wa Mallya.

Wengine ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Simon Kiles Samwel, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Solomoni Shati na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote.

 Mwenyekiti Kiles akitoa heshima za mwisho

 Mwenyekiti Komote akitoa heshima za mwisho

Akitoa salamu za rambirambi, Ngicho ameeleza kusikitishwa na kifo hicho na kwamba amelazimika kuahirisha kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Tarime kwa ajili ya kushiriki tukio la kuaga mwili wa Mallya.

Frederick Mallya wakati wa uhai wake

DC Mntenjele amesema “Tumesikitishwa na kifo hiki.” Huku Mwenyekiti Kiles akisema “Hili ni pigo kubwa kwetu kama halmashauri.”

#MaraOnlineNews-Updates

2 comments:

  1. Umevipigana vita vikuu ,mwendo umeumaliza pumzika ndugu yetu😭🙏

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages