NEWS

Tuesday 11 January 2022

MAJONZI: Wanahabari 5 wa mkoani Mwanza wafa ajalini Simiyu



WAANDISHI wa habari watano ni miongoni mwa watu 14 walithibitika kupoteza maisha katika ajali mbaya ya magari iliyotokea leo asubuhi barabara kuu ya Mwanza – Musoma, wilayani Busega, Simiyu.

Ukiacha Paul Salinga ambaye alikuwa dereva wa gari walilokuwa wakisafiria, wanahabari waliotajwa kufariki dunia ni Johari Shani wa Uhuru Digital na Husna Mlanzi wa ITV Mwanza.

Wengine ni Anthon Chuwa wa Habari Leo Digital, Abel Ngapemba (Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) na Steven Msengi (Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe).

Inaelezwa kuwa gari la serikali (pichani juu) lililokuwa limewabeba wanahabari hao liligongana na Hiace ya abiria uso kwa uso, ambapo pia waandishi wa habari, Tunu Herman (Freelancer) na Vany Charles (ITV Mwanza) wamepata majeraha.



Wanahabari hao walikuwa sehemu ya msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel ambaye ilikuwa aende wilayani Ukerewe kukabidhiwa kwa niaba ya serikali miradi ya kijamii iliyokamilishwa.

Kutokana na msiba huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi, akiwapa pole na kuwatakia wanafamilia, ndugu na jamaa wa marehemu hao moyo wa uvumilivu kipindi hiki cha majonzi makubwa.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages