NEWS

Sunday, 9 January 2022

Mbunge Ghati kutoa milioni 10 kugharimia ujenzi nyumba ya UWT Mara



MBUNGE wa Viti Maalum, Ghati Zephania Chomete (pichani juu kulia) ameahidi kutoa mchango wa Sh milioni 10, kugharimia ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mara na jengo la kitega uchumi, kwa ustawi wa wanawake mkoani.

Mbunge huyo wa mkoa wa Mara ametoa ahadi hiyo leo Januari 9, 2022 mbele ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudentia Kabaka (pichani juu kushoto) na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya jumuiya hiyo mkoani Mara.



Ujenzi huo utaanza wakati wowote kuanzia sasa, baada ya Mbunge Ghati kukabidhi mchango wa mamilioni hayo ya fedha.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages