MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, jana Januari 19, 2022 amezuru Shule ya Sekondari ya Tegeruka jimboni, kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Katika ziara hiyo, Mbunge Muhongo amekuta wanafunzi wa kidato cha kwanza waliokwisha kuripoti hadi jana, yaani siku ya tatu tangu shule zifunguliwe, ni 54 kati ya 184 waliochaguliwa kujiunga na kidato hicho shuleni hapo mwaka huu.
Profesa Muhongo aliyesimama akikagua chumba kipya cha darasa shuleni hapo |
Pamoja na mambo mengine, Profesa Muhongo amepiga picha kadhaa akiwa pamoja na wanafunzi hao, wazazi na walimu.
Shule ya Sekondari ya Tegeruka ilikuwa ya kwanza jimboni hapa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 60 zilizopatikana kwa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni mkopo uliotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya mapambano dhidi ya UVIKO-19 nchini.
Jimbo la Musoma Vijijini tunatoa shukrani ngingi sana kwa Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan,” Profesa Muhongo amesema.
(Imeandikwa na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment