NEWS

Saturday 8 January 2022

Rais Samia afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri Tanzania




RAIS Samia Suluhu Hassan (pichani juu) amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri Tanzania.

Akitangaza mabadiliko hayo jijini Dar es Salaam jioni ya leo Januari 8, 2022, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais pia amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Mawaziri wapya watano walioteuliwa na wizara zao zikiwa kwenye mabano ni Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), DkT Pindi Chana (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt Anjeline Mabula (Ardhi) na Hussein Bashe (Kilimo).

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, George Simbachawene ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria iliyokuwa inaongozwa na Profesa Palamagamba Kabudi.

Kabla ya mabadiliko hayo, Wizara ya Ardhi ilikuwa inaongozwa na William Lukuvi, sasa itaongozwa na aliyekuwa Naibu wake, Dkt Angeline Mabula.

Naibu mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Samia ni Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages