RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Mhifadhi William Simon Mwakilema (pichani juu) kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Mhifadhi Mwakilema anachukua nafasi ya Mhifadhi Dkt Allan Herbert Kijazi, ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kabla ya uteuzi huo, Mhifadhi Mwakilema alikuwa Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA.
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu, uteuzi huo wa Mhifadhi Mwakilema, umeanza Januari 8, 2022.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment