NEWS

Sunday 2 January 2022

Simanzi: Afisa Mipango Tarime Vijijini afariki duniaAFISA Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Fredrick Mallya (pichani juu) amefariki dunia akitibiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri hiyo, Solomoni Shati ametangaza kifo cha Mallya leo Jumapili asubuhi.

“Heri ya mwaka mpya viongozi, kwa masikitiko makubwa naomba niwataarifu kuwa Afisa Mipango wangu, ndugu Fredrick Mallya amefariki muda huu akiwa anapatiwa matibabu Bugando,” DED Shati amesema katika ujumbe wake alioutuma kwenye group la Whatsapp la CCM Wilaya ya Tarime.

Dakika chache baadaye, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Simon K Samwel naye ameandika katika group hilo akielezea kifo cha Mallya.

“Halmashauri tumepata msiba, Afisa Mipango Mallya amefariki leo,” K amesema.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho ameeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho na kutoa salamu za pole, huku akiitakia familia ya Mallya na watumishi wote wa halmashauri hiyo moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wao.

#MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages