NEWS

Thursday 6 January 2022

Spika Ndugai ajiuzulu
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai (pichani juu) ametangaza kujiuzulu wadhifa huo.

Katika barua yake aliyoandika kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Januari 6, 2022, Ndugai amesema amefanya uamuzi huo binafsi kwa hiari yake na kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa, Serikali na chana chake - CCM.

"Nakala ya barua yangu hiyo ya kujiuzulu nimeiwasilisha kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya hatua stahili kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na Sheria nyingine husika ili kuwezesha mchakato wa kumpata Spika mwingine uweze kuanza,

"Nachukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wabunge wenzangu, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali kwa ujumla, wananchi wa jimbo langu la Kongwa na Watanzania wote kwa ushirikiano mkubwa mlionipa katika kipindi chote nilipokuwa Spika wa Bunge letu tukufu," Ndugai amesema katika barua hiyo aliyoisaini na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages