NEWS

Friday 4 February 2022

Boti zaandaliwa kupeleka wakazi wa kisiwa cha Rukuba sherehe za CCM
BOTI mbili zimeandaliwa kusafirisha wakazi wa kisiwa cha Rukuba kwenda kushiriki sherehe za CCM zitakazofanyika kitaifa mjini Musoma, kesho Februari 5, 2022.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo za kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM, ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kisiwa cha Rukuba ni mojawapo ya vijiji vitatu vinavyounda kata ya Etaro katika jimbo la Musoma Vijijini linaloongozwa na Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Sospeter Muhongo

Wakazi wa kisiwa hicho wanaendelea kumshukuru Rais Samia kwa kuwapatia shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuwajengea kituo cha afya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa cha Rukuba, Japhari Ibrahim Kabasa, tayari ujenzi wa mradi huo umeanza, ambapo wananchi kisiwani hapo wamechangia nguvu kazi ya kuchimba misingi ya majengo yote, kusoma mawe, kokoto na maji.

Serikali ya kijiji/kisiwa hicho imetumia mapato yake kununua vifaa vya ujenzi, zikiwemo pampu mbili za kuvutia maji kutoka Ziwa Victoria, mipira yake na mapipa ya kutunzia maji ya ujenzi.

Aidha, fedha za mkopo kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zilizotolewa na Serikali kupitia kampeni ya kupambana na UVIKO-19, zimeanza kutumika kununua saruji mifuko 599, nondo 210, mbao 32 na dawa ya kuua mchwa.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages