NEWS

Wednesday 2 February 2022

Chongolo azindua tawi la CCM Tarime, balozi wa mtaa atumia fursa kupata baiskeliKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo (pichani juu katikati), leo Februari 2, 2022 amezuru wilayani Tarime, Mara na kupata fursa ya kuzindua tawi jipya la mtaa wa Buhemba.

Katika ziara hiyo, Chongolo amekaribishwa na mwenyeji wake, Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki aliyefuatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho na Mkuu wa Wilaya, Kanali Michael Mntejele na makada wengine wa chama hicho tawala.

Mbunge Kembaki (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo

Katibu Mkuu huyo wa CCM amemshukuru Balozi wa Mtaa huo kwa juhudi kubwa alizofanya kuhamasisha na kuwezesha wanachama wapya 100 kujiunga na chama hicho katika kipindi kifupi.

Chongolo ametumia nafasi hiyo pia kuwataka viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Balozi wa Shina hilo alitumia nafasi hiyo kuomba usafiri wa baiskeli ili kumwezesha kuwafikia wananchi wengi kuhamasisha chama, ambapo umeitishwa mchango wa dharura zikapatikana fedha akapewa shilingi 200,000.

(Habari na picha zote: Geofrey John)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages