KATIBU Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (pichani juu), jana amesaini mikataba sita yenye thamani ya shilingi bilioni 34.7 inayohusu sekta ya maji.
Mikataba hiyo inahusisha kampuni tano; ambazo ni M/S PRD Rigs Tanzania Ltd, M/S Equiplus Company Ltd, M/S GF Trucus and Equipments Ltd, Bing Bang Machines and Parts Ltd na Mantrack Tanzania Ltd.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo, mikataba hiyo ni kuhusu ununuzi wa mitambo ya uchimbaji wa mabwawa na visima, vifaa vya uchunguzi wa maji chini ya ardhi, mashine za kuchimba miamba na pampu.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment