NEWS

Monday, 7 February 2022

Msanii Mrisho Mpoto aula Wizara ya Maji



MSANII nguli wa muziki nchini, Mrisho Mpoto (pichani juu kulia) ameteuliwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuwa Balozi wa Sekta ya Maji Tanzania.

Waziri Aweso amefanya uteuzi huo leo Februari 7, 2022 baada ya msanii huyo kuimba wimbo wenye maudhui bora na uliosheheni takwimu sahihi kuhusu sekta ya maji, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Bunda mkoani Mara, iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.


Rais Samia (wa pili kulia) wakati wa uwekeji jiwe la msingi kwenye mradi huo

Waziri Aweso

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo jioni na Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Wizara ya Maji, Florence Temba, msanii Mpoto atakuwa akitangaza sekta ya maji kupitia kazi yake ya Sanaa katika shughuli mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali.

Taarifa hiyo imemtaja Mrisho Mpoto kama mmoja wa wasanii bora wa muziki katika ukanda wa Afrika Mashariki, aliyebobea katika kutumia vionjo vya asili kufikisha ujumbe kwa hadhira.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages