NEWS

Wednesday 9 February 2022

Profesa Muhongo aweka wazi mamilioni ya Mfuko wa JimboMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani juu) ametangaza kupokea shilingi milioni 52.43 za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa jana, fedha hizo zitaelekezwa kwenye ujenzi wa maabara za Fizikia, Kemia na Baiolojia, maktaba na vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule za sekondari.

“Wakuu wa sekondari wakishirikiana na madiwani wao watume maombi yao kwa Afisa Mipango wa Halmashauri. Maombi yao yawe yamefika kwake kabla ya Februari 28, 2022.

“Nitaitisha kikao cha kugawa fedha hizo Machi 2022, tarehe itatangazwa,” Profesa Muhongo amesema.

Mbunge huyo amefafanua kuwa utaratibu utakaotumika ni wa kuzipatia shule husika vifaa vya ujenzi, sio fedha taslimu.

“Wanunuzi wa vifaa vya ujenzi ni halmashauri yetu. Kwa hiyo, fedha za Mfuko wa Jimbo hazitolewi ndani ya halmashauri,” ameongeza.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages