MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Hapi (pichani juu) amewataka madiwani kutojihusisha kufanya biashara na halmashauri zao, huku akisisitiza kuendeleza operesheni ya kuwashughulikia watumishi wanaokwamisha juhudi zinazofanywa na serikali kuwaletea wananchi maendeleo ya kisekta mkoani.
“Viongozi wakae mbali na miradi ya maendeleo. Ukiingia 18 zangu nitakufyeka hadharani,” RC Hapi amesisitiza.
Aidha, RC huyo amewaonya wakuu wa idara wanaoendelea kufanya mawasiliano ya kikazi na watumishi alioagiza kusimamishwa kazi katika halmashauri za mkoa huo kuacha kufanya hivyo.
Tayari ameagiza watumishi wengine wanne kuondolewa kwenye nafasi zao haraka katika Halamshauri ya Wilaya ya Tarime (Vijiini), kutokana na tuhuma zinazowakabili, ikiwemo ubadhirifu wa fedha za umma.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa maelekezo hayo juzi, wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara wa wafanyabiashara na wakazi wa mji mdogo wa Sirari uliopo wilayani Tarime, mpakani na nchi ya Kenya.
Kwa habari kamili kuhusu maagizo ya RC Hapi na mengine mengi yaliyojiri katika mkutano huo, soma gazeti la Sauti ya Mara wiki hii.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment