NEWS

Wednesday 16 March 2022

Ardhi Mara watoa elimu ya ulipaji kodi nyumba kwa nyumba



OFISI ya ardhi mkoa wa Mara imepita nyumba kwa nyumba kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi na pango kwa wakati.

Akizungumzia mpango huo unaoendelea katika Halmashauri ya Manispaa Musona na maeneo mengine mkoani, Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Mara, Happyness Mtutwa amesema kazi hiyo inaendelea vizuri na kwamba lengo in kumfikia kila mdaiwa.

Mtutwa amesema wameamua kupita kila nyumba na kutoa elimu na kusambaza dodoso na notisi za ulipaji.

Kamishna huyo amesema wameona watoe elimu hiyo kabla ya kuchukua hatua nyingine na kwamba wananchi wamekuwa wakiitikia kulipa kodi.

Amesema kwamba baada ya kazi hiyo, watakaokaidi kulipa madeni yao ya kodi ya ardhi ya pango watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

“Tumeamua kufanya zoezi la utoaji elImu kwa kupita kila nyumba ili kila mmoja apate uelewa juu ya kodi hii na tutamfikia kila mmoja.

"Tunawakumbusha wananchi kulipa kodi ya ardhi kwa wakati na kuacha kulimbikiza na kufikia deni kubwa litakalowafanya kushindwa kulipa," amesema Mtutwa.

Baadhi ya wananchi waliofikiwa kupewa elimu hiyo katika kata za Nyasho na Makoko, Manispaa ya Musoma, wamesema imewasaidia kupata uelewa.

Wamesema mwanzoni wamekuwa wakichanganya na kodi ya pango inayokuwa inatozwa kwenye tozo za simu wakidhani ndio kodi ya ardhi.

(Imeandikwa na Shomari Binda, Musoma)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages