NEWS

Saturday 19 March 2022

CCM yaridhishwa utekelezaji miradi Tarime Vijijini, yasisitiza ushirikishajiKATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Lengaeli Akyoo amefanya ziara ya siku mbili kutembelea na kukagaua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Tarime na kusisitiza umuhimu wa dhana shirikishi wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.

“Ninaona suala la ushirikishaji bado ni tatizo. Kwanini hizi kamati na wananchi hawashirikishwi ikiwa miradi inayojengwa ni kutokana na tozo zao, hii miradi ni ya wananchi wanatakiwa watambue kila hatua,” Akyoo amesisitiza.

Hata hivyo, akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Akyoo ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi mikubwa, baada ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa mamilioni ya fedha kuigharimia.

Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa kituo cha afya Bumera, Shule ya Sekondari Nyasaricho, jengo la Halmashauri ya Wilaya na mradi wa maji katani Sirari.“Niwashukuru sana viongozi kuanzia Mwenyekiti wa Halmashauri, Simon Kiles, kwa kuendelea kusimamia miradi hii na kwa kweli mmefanaya kazi nzuri sana,” amesema Akyoo aliyefuatana na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkuu wa Wilaya, Kanali Michael Mntejele, Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Valentine Maganga na wenyeviti wa halmashauri zote mbili za wilaya hiyo.

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na viongozi hao kwa upande wa Halmashauri ya Mji wa Tarime ni jengo la utawala la halmashauri hiyo, ujenzi wa Shule ya Sekondari Gicheri, mradi wa maji Gimenya, matengenezo ya barabara kwa kiwango cha changarawe, kituo cha afya Kibumaye na Shule ya Sekondari Magena inayojengwa na makundi rika (saiga) katani Nkende.

Hata hivyo, Katibu huyo wa CCM Mara na viongozi aliofuatana nao wameonesha kutoridhishwa na ubora wa baadhi ya miradi katika Halmashauri ya Mji wa Tarime na kuagiza hatua zichukuchuliwe dhidi ya watakaobanika kutekeleza miradi hiyo chini ya viwango.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages