NEWS

Tuesday 8 March 2022

Mwenyekiti Halmashauri ya Serengeti akagua ujenzi wa madarasa shule za sekondari


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Ayub Mwita Makuruma (pichani juu kulia), leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari.

Katika ziara hiyo, Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe, amefuatana na Afisa Utumishi Msaidizi, Afisa Elimu Sekondari na Mhandisi wa Halmashauri hiyo.Shule za sekondari ambazo Mwenyekiti huyo ametembelea na kuhimiza uharakishaji na ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ni Gesarya, Nyansurura, Kisaki, Iseresere na Majimoto.Ujenzi wa vyumba hivyo unagharimiwa na fedha ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliomba mkopo kwa ajili ya mapambano dhidi ya janga la UVICO-19 nchini.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages