NEWS

Tuesday 8 March 2022

TPO Tarime watoa msaada kwa shule za Sabasaba, Borega ‘B’


Viongozi wa TPO wilaya ya Tarime wakikabidhi msaada

Taasisi ya Kizalendo Tanzania(TPO) jana imetoa msaada wa vitu mbalimbali katika shule za msingi Sabasaba na Borega ‘B’ zote za wilayani Tarime, Mara.

Mwenyekiti wa TPO Mkoa wa Mara , Dkt Emmanuel Obimbo alifuatana na Mwenyekiti wa TPO Wilaya ya Tarime Philipo Lusotola kukabidhi msaada huo ambao ni pamoja na miche ya sabuni 100, madaftari na kalamu  .

Watoto wanaoishi katika mazingira magumu walipewa kipaumbele katika zoezi hilo.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo Dkt Obimbo alitumia fursa hiyo kuhimiza uzalendo kwa walimu na wanafunzi katika shule hizo.

“Tunajifunza kutoka kwa Hayati Baba wa Taifa Mwl.Nyerere alivyojitoa yeye Mwenyewe pamoja na baadhi ya wazee wa Tanzania hii kutuletea uzalendo kwa kutushirikisha pamoja Watanzania kuwa kitu kimoja” alisema Dkt Obimbo ambaye ni Mwenyekiti wa TPO Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa TPO Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa , Dkt Emmanuel Obimbo akikabidhi msaada huo kwa baadhi ya wanafunzi

Viongozi hao wa TPO walihimiza pia elimu ya uzalendo kuendelea kutolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Walimu na wanafunzi wa shule hizo walishukuru taasisi hiyo kwa kuwatembelea wakisema ni mfano mzuri wa kuigwa.

(Picha na Habari Gitano Moremi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages