NEWS

Friday 11 March 2022

TASAF yawatembelea wanufaika wake Tarime Vijijini



WANUFAIKA wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), wameishukuru serikali kuendelea kuwajali, kuwakwamua kiuchumi na kuwawezesha kuondokana na umaskini.

Wametoa pongezi hizo Machi 11, 2022 walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, maofisa wa TASAF makao makuu na waratibu wa mfuko huo kutoka halmashauri hiyo.

“Ninaishukuru sana serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za mpango wa TASAF maana zimetufaa sana. Nimeweza kununua vifaa vya shule kwa ajili ya watoto, kujenga na hata huyu ng’ombe ametokana na fedha za mpango huu,” amesema Modesta Chacha, mkazi wa kijiji cha Kemakorere.


Modesta akionesha ng'ombe aliyempata kwa uwezesho wa TASAF

Kwa upande wake, DC Mntenjele amewashukuru walengwa hao kwa kutumia fedha za TASAF vizuri na kuwataka waratibu kutoa elimu endelevu juu ya matumizi sahihi ya fedha hizo.

“Tuendelee kuwahimiza juu ya matumizi mazuri ya fedha hizi, walengwa wahakikishe watoto wanapata mahitaji ya shule na walio chini ya miaka mitano kupelekwa kliniki kama ilivyokusudiwa,” amesema.

Nao Afisa Mfuatiliaji kutoka TASAF Makao Makuu, Kobeche Wambura na Mratibu wa Mfuko huo Wilaya ya Tarime (Vijijini), Emmanuel Kadama wameweka wazi kuwa mpaka sasa halmshauri hiyo ina wanufaika 6,606 katika vijiji 88.

“Ninawahimiza wanufaika waendelee kutumia fedha hizi vizuri, ili hata kama mpango huu utaisha uweze kuacha alama katika maisha yao,” Kadama amesisitiza.

(Habari na picha zote: Geofrey John)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages