NEWS

Saturday 12 March 2022

DC Mntenjele awapongeza wanufaika wa TASAF Tarime Mji



MKUU wa Wilaya (DC) ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele (pichani juu mbele) amewapongeza wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kuzitendea haki fedha za mfuko huo.

DC Mntenjele ameyasema hayo Machi 11, 2022 wakati wa ziara yake ya kuangalia maendeleo ya wanufaika wa fedha zilizotolewa na TASAF) katika halmashauri hiyo.

Amesema wanufaika wa fedha hizo wameanzisha miradi mbalimbali ya kuwakwamua kiuchumi na kuwaondolea umaskini.

Hata hivyo, mkuu huyo wilaya amewataka kuzingatia malezi bora kwa watoto wao kwani nao ni hazina.

“Nawapongeza sana kwa maendeleo mnayoyafanya, lakini zingatieni na malezi ya watoto, hakikisheni wanaenda shule na kwa watoto wenye umri unaotakiwa kwenda kliniki wapelekwe ili wakue na afya njema, maana nao ni hazina,” amesisitiza.

Naye Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji wa Tarime, Desmond Basaya amesema wana walengwa 1,767 ambao baadhi yao wanatumia fedha hizo kuendesha kilimo, ufugaji na biashara ndogo ndogo.

Mmoja wa wanufaika wa TASAF katika halmashauri hiyo, Bernard Paul kutoka kata ya Nyandoto, ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha hizo, akisema zimemwezesha kujenga nyumba na mtaji wa biashara ya majiko.

Benard akielekeza sehemu anayotumia kutengeneza majiko

“Naomba Mungu aendelee kumbariki Rais wetu, fedha za TASAF zimenitoa kwenye dimbwi la umaskini, angalau sasa hivi ninaishi maisha mazuri. Nimeweza kupeleka watoto shuleni na kujenga nyumba ya kudumu na kuanzisha biashara,” amesema mkazi wa kata ya Ketare, Kadogo Charles ambaye pia ni mnufaika wa TASAF.

Kadogo (mbele) akielezea TASAF ilivyomnufaisha

(Habari na picha zote: Asteria John)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages