NEWS

Tuesday 1 March 2022

Waziri Aweso aagiza gharama za huduma ya maji Karatu zipitiwe upya


WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso (pichani katikati juu), jana amefanya ziara maalumu ya kikazi katika mji wa Karatu na kuagiza gharama za huduma ya maji kwa wakazi wa mji huo zipitiwe upya.

Waziri Aweso amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa na kubaini kuwa bei ya huduma ya maji katika mji huo ni kubwa, huku upangaji wake ukikosa vielelezo muhimu.

Amesema serikali inatuma timu ya wataalamu wa sekta ya maji kuangalia uhalisia wa gharama za huduma ya maji zinazotozwa kwa wateja mbalimbali mjini Karatu.

Waziri huyo ameongeza kuwa serikali itafanya mabadiliko makubwa ya utendaji na utoaji huduma ya maji kutokana na ukaguzi alioufanya ofisi za Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA).

Awali katika ziara hiyo, Waziri Aweso alizindua mradi wa uhifadhi chanzo cha maji chemchemi za Quang’dend, mito Mang’ola na Baray wilayani Karatu.

Waziri Aweso (mwenye koti jeusi katikati) akikagua mradi huo mara baada ya uzinduzi

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages