NEWS

Saturday 9 April 2022

Makumbusho ya Baba wa Taifa yawaita Watanzania Butiama


MKURUGENZI wa Makumbusho ya Mwalimu Julius K. Nyerere (Baba wa Taifa) yaliyopo Butiama, Emmanuel Kiondo (pichani) ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki shereheza za Madhimisho ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yatakayofanika April 13, 2022 (Jumatano ijayo) kwenye viwanja vya Mwenge kijijini Butiama.

Kiondo amesema pamoja na mambo mengine, Makumbusho hiyo imeanda onesho lenye mvuto wa aina yake lililosheheni historia ya Mwalimu Nyerere ambaye licha ya kwamba hayuko hai, bado mawazo, falsafa na mitazamo yake kwa taifa vinaishi.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages