NEWS

Saturday 9 April 2022

RUWASA waanza maandalizi ya kuchimba visima vya maji Butiama na Rorya



WATAAAM kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Makao Makuu, wameanza upimaji wingi wa maji katika baadhi ya maeneo ya wilaya za Butiama na Rorya mkoani Mara, kwa ajili ya kuchimba visima vya maji.



Hatua hiyo ni utekelezaji wa moja ya mapendekezo ya Kamati ya Kitaifa iliyochunguza uchafuzi wa maji ya Mto Mara. Lengo ni kuwezesha wakazi wa maeneo hayo kupata huduma ya maji ya visima.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Wegero wilayani Butiama ameishukuru Serikali kwa mpango huo akisema utawaongezea wanakijiji wigo wa kupata huduma ya maji.



Wakazi wa kijiji hicho wamesema tangu kutokea kwa tukio la uchafuzi wa maji ya Mto Mara katika eneo la Kirumi darajani, kumekuwa na shida kubwa ya maji kwenye maeneo mengi kijijini hapo.

“Kuwepo kwa mpango huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo hilo, lakini pia kuwasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kutafuta maji,” amesema mkazi wa kijiji hicho, Chacha Joseph.



Pia, wananchi hao wameishukuru RUWASA na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa zinazofanywa kuwaboreshea wananchi wa vijijini huduma ya maji.

“Ninamshukuru sana Rais Samia kwa jinsi anavyosaidia akina mama kuondokana na tatizo la maji, ninaomba wasaidizi wake wamsaidie kwa kufanya kazi kwa bidii,” amesema mwanakijiji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Nyakia Werema.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages