NEWS

Sunday 10 April 2022

Wananchi waishio jirani na hifadhi watakiwa kujiandaa kisaikolojia kukutana na wanyamapori wakaliSimba

WANANCHI wanaoishi jirani na hifadhi za wanyamapori wametakiwa kujiandaa kisaikolojia kuwa na maisha ya kukutana na wanyamapori wakali na waharibifu muda wowote.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ametoa kauli hiyo mjini Musoma jana Aprili 9, 2022, wakati wa kikao cha kupeana uelewa juu ya Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu vijiji 975 nchini katika ziara ya mawaziri wa kisekta.


Tembo

“Nampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maamuzi ya kuruhusu baadhi ya maeneo kupewa wananchi, niweke angalizo wananchi wajiandae kisaikolojia kukutana na wanyama wakali na waharibifu, hasa tembo, simba, chui, n.k,” Masanja amesema.


Chui

Aidha, Naibu Waziri Msanja amewataka wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wa vijiji kuwapa wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi elimu ya uhifadhi ili kupunguza migogoro ya binadamu na wanyama wakali na waharibifu.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages