NEWS

Wednesday, 6 April 2022

Waziri Aweso apangua uongozi Mamlaka ya Maji Singida



WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso (pichani), leo Aprili 6, 2022 amefanya mabadiliko ya uongozi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mji Singida (SUWASA).

Katika mabadiliko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA, Mhandisi Patrick Nzamba amehamishiwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama-Shinyanga (KASHWASA), kuchukua nafasi ya Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye amestaafu utumishi wa umma.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji Dodoma (DUWASA), Sebastian Warioba amepangiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA.

“Waziri Aweso alimteua Warioba kuwa mkurugenzi mapema Januari 2022,” imeeleza taarifa kwa umma iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maji, Florence Temba.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages