NEWS

Tuesday 26 July 2022

Kampeni kabambe ya Sensa ya Watu na Makazi yaja Musoma VijijiniMbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo.

Na Mwandishi Wetu, Musoma Vijijini
-------------------------------------------------

JIMBO la Musoma Vijijini mkoani Mara limejipanga kufanya kampeni ya siku 24 ya kuhamasisha wananchi wake kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi.

Sensa ya Watu na Makazi itafanyika nchini kote siku ya Jumanne Agosti 23, mwaka huu.

Kampeni hiyo ya Musoma Vijijini itaratibiwa na ofisi ya Mbunge Profesa Sospeter Muhongo na itafanyika katika kata zote 21 zinazounda jimbo hilo kuanzia Julai 30 hadi Agosti 22, mwaka huu.

“Uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika siku ya Jumamosi Julai 30, 2022 kuanzia saa 9:00 alasiri kijijini Busekera,” imeeleza taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi ya Mbunge leo.

Kulingana na taarifa hiyo, viongozi watakaongoza kampeni hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt Khalifan Haule, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Msongela Palela na Mbunge Muhongo.

Taarifa hiyo imetaja vikundi vya uhamasishaji vilivyotayarishwa na Mbunge huyo kuwa ni kwaya za Bugoji na Kiriba.

Vikundi vingine ni ngoma za asili za Lirandi Bugwema, Kiwanjuki Kiriba, Mbegete Nyakatende na Nyakatende Mtelezo Show.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages