NEWS

Sunday 3 July 2022

Luoga avuta fomu ya kuwania Uenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM TaifaKADA wa chama tawala - CCM, Glorious Luoga (katikati pichani juu), amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa Wazazi ya chama hicho ngazi ya Taifa.

Luoga alichukua na kuijaza fomu hiyo, kisha kuirejesha katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Dodoma, jana.

Luoga (kulia) akiwa katika harakati hizo kwenye ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Umoja wa Wazazi jijini Dodoma

Itakumbukwa kuwa Luoga amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Bara, Mwanasheria na Afisa Maadili wa CCM.

Pia Luoga amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime katika Serikali ya wamu ya Nne na Awamu ya Tano.

Glorious Luoga akiwa na fomu ya kuwania Uenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM Taifa

Akihudumu kama DC Tarime, alionesha utumishi uliotukuka, kama vile kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa wakati na kusimamia kwa ufanisi maendeleo ya kisekta katika wilaya hiyo ya mkoani Mara.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages