NEWS

Saturday, 20 June 2026

Jeshi la Polisi lathibitisha kifo cha RPC Tabora SACP Abwao



Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, amethibitisha kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao (pichani).

SACP Abwao amefariki dunia leo Jumamosi, Juni 20, 2026, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa akiendelea na matibabu.

DCP Misime amesema SACP Abwao amefariki dunia baada ya kuugua na kuwa chini ya uangalizi wa madaktari katika hospitali hiyo.

"Ni kweli aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao, amefariki dunia leo tarehe 20 Juni 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu," amesema.

Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ugonjwa wake na ratiba za mazishi zitatolewa na familia pamoja na mamlaka husika.

Akizungumzia msiba huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amesema kifo cha SACP Abwao ni pigo kubwa kwa Jeshi la Polisi na wananchi wa mkoa wa Tabora kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha usalama, amani na utulivu wa mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages