NEWS

Wednesday 27 July 2022

Rais Samia ateua Ma-RC wapya 9, Hapi atupwa nje, Dkt Chegeni RC mpya Mara, Malima apelekwa MwanzaAlly Salum Hapi

Na Mara Online News
---------------------------

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa wapya tisa na kutengua uteuzi wa wengine, akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Salum Hapi.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dodoma, Zuhura Yunus leo Julai 28, 2022, imewataja Wakuu wa Mikoa wapya kuwa ni Dkt Raphael Masunga Chegeni aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Wateule wengine na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido, Nurdin Hassan Babu (Kilimanjaro), Fatma Abdallah Mwasa (Morogoro) na Halima Omari Dendego (Iringa).

Wengine ni Peter Joseph Serukamba (Singida), Kanali Ahmed Abbas Ahmed (Mtwara), Kanali Laban Elias Thomas (Ruvuma), Albert John Chalamila ((Kagera) na Dkt Yahaya Esmail Nawanda (Simiyu).

Wakuu wa Mikoa waliohamishwa na mikoa yao mipya ikiwa kwenye mabano ni Anthony John Mtaka (Njombe), Queen Cuthbert Sendiga (Rukwa) na Waziri Waziri Kindamba (Songwe).

Wengine ni Omary Tebweta Mgumba ambaye amehamishiwa mkoa wa Tanga, Martin Reuben Shigella (Geita), Adam Kighoma Malima (Mwanza) na Rosemary Staki Senyamule (Dodoma).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages