NEWS

Thursday 28 July 2022

RAS Msovera naye bye bye MaraMsovera Albert Gabriel

KAMA alivyofanya kwa Wakuu wa Mikoa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine.

Kulinga na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dodoma, Zuhura Yunus leo Julai 28, 2022, Makatibu Tawala waliohamishwa ni pamoja na Msovera Albert Gabriel ambaye amepelekwa Mkoa wa Kigoma akitokea Mkoa wa Mara.

Aidha, Rais Samia amemhamisha aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

Hivyo ofisi ya mkoa wa Mara sasa inakuwa na viongozi wapya, baada ya Rais Samia pia kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Ally Salum Hapi na kumteua Dkt Raphael Masunga Chegeni kuchukua nafasi hiyo.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages