NEWS

Friday 19 August 2022

Madiwani Tarime Vijijini wachagua Makamu Mwenyekiti na Wenyeviti wa KamatiKutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Peter Ntogoro Kurate, Mwenyekiti Simion Kiles Samwel na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Solomon Shati.

Na Mara Online News
-----------------------------

DIWANI wa Kata ya Mwema, Peter Ntogoro Kurate (CCM), amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), akichukua nafasi ya Victoria Mapesa aliyemaliza muda wake.

Uchaguzi huo umefanyika katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Simion Kiles Samwel, leo Agosti 19, 2022.

Aidha, wenyeviti wa kamati mbalimbli za halmashauri hiyo wamechaguliwa katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya JK Nyerere, Nyamwaga.Picha zote na Mara Online News

Baadhi ya wenyeviti hao ni Steven Gibayi (Elimu, Afya, Maji na Maendeleo ya Jamii), Godfrey Kigoye (Uchumi, Ujenzi na Mazingira), Ngocho Wangwe (Maadili) na Kiles anayeendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango.

Makamu Mwenyekiti, Kurate na wenyeviti wa kamati waameahidi kushirikiana na Mwenyekiti Kiles, madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Solomon Shati na watumishi wa halmashauri hiyo katika utekelezaji wa majukumu ya kuwatumikia wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages