NEWS

Thursday 4 August 2022

Mbunge Muhongo ashusha msaada wa saruji kutekeleza miradi ya afya na elimu katani Bukumi


Wasaidizi wa Mbunge Profesa Sospeter Muhongo wa Musoma Vijijini wmekabidhi saruji mifuko 200 katani Bukumi, jana Agosti 3, 2022.

Na Mwandishi Wetu, Musoma Vijijini
----------------------------------------------

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa msaada wa saruji mifuko 200 kuchangia ujenzi wa zahanati tatu na vyumba viwili vya madarasa katika kata ya Bukumi.

Wasaidizi wa Mbunge Muhongo wamekakabidhi msaada huo jana Agosti 2, 2022, ambapo kila zahanati imepewa mifuko 50 na mingine 50 imeelekezwa kwenye ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya Shule ya Msingi Busekera.

Diwani wa Kata ya Bukumi, Munubhi Musa amechangia ujenzi huo kwa kutoa shilingi 100,000 kwa kila zahanati.

Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne; ambavyo ni Buira, Bukumi, Buraga na Busekera, ina zahanati moja iliyopo kitongoji cha Kurugee kijijini Buraga.

Kwa mujibu wa ofisi ya Mbunge, vijiji vingine vitatu vimeamua kujenga zahanati zake na ujenzi tayari umeanza kwa kasi ya kuridhisha.

Michango ya wanavijiji katika ujenzi wa miradi hiyo ni nguvukazi na shilingi 10,000 hadi 15,000 kwa kila kaya.

“Wakazi wa kata ya Bukumi na rafiki zetu tunaombwa tujitokeze kuchangia miradi hii ya ujenzi iliyoanzishwa na inatekelezwa kwa nguvukazi na michango ya fedha taslimu kutoka wanavijiji,” amesema Mbunge Muhongo.

Profesa Sospeter Muhongo

Michango mingine ya Mbunge Muhongo kwenye sekta ya afya ndani ya kata hiyo ni pamoja na gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa zahanati ya Kurugee.

Pia saruji mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Bukumi inayojengwa katika kitongoji cha Kukema Burungu.

Jimbo la Musoma Vijijini linaundwa na kata 21 zenye vijiji 68.

Lina Hospitali ya Wilaya inayoendelea kujengwa, vituo vitatu vya afya, zahanati 23 za Serikali na nne za binafsi.

Aidha, ujenzi wa vituo vitatu vya afya na zahanati katika vijiji 17 unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages