
Rochi Shaban Mkolekuwa enzi za uhai
Na Mwandishi Wetu
Musoma
------------
Meneja wa Ubora wa Maji katika Maabara ya Mkoa wa Mara, Rochi Shaban Mkolekuwa (39), mke wake, Mariam Msigwa (34) na mtoto wao, Rochi Shaban (miaka minne), wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto ndani ya nyumba yao usiku wa kuamkia Jumatatu, Januari 5, 2026.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika Manispaa ya Musoma, na kwamba uchunguzi umeanza ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
"Mwili wa baba ulikutwa sebulenina miili ya mama na mtoto ilikutwa chumbani. Tumeanza uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine," amesema Magere.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki, akieleza kusikitishwa na kifo cha mtumishi huyo pamoja na familia yake. "Tunamwomba Mwenyezi Mungu awape marehemu pumziko la amani, Amina," Waziri Aweso katika taarifa yake kwa umma.
No comments:
Post a Comment