NEWS

Wednesday 31 August 2022

Profesa Muhongo amnusuru kijana kukosa masomo ya kidato cha tano, amsaidia mahitaji ya vifaa vyote na nauli ya kwenda shuleMsaidizi wa Mbunge, Vaileth Peter (kushoto) na kijana Jastine Mgaya Bina, wametoka benki kufanya malipo ya shule na tayari wamemaliza kununua vifaa vya shule, vikiwemo vitabu vinavyohitajika.

Na Mara Online News
------------------------------

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, amempatia kijana Jastine Mgaya Bina kutoka kijiji cha Kaburabura, kata ya Bugoji jimboni humo, msaada wa mahitaji yote ya kuanza masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Nyakato iliyopo Bukoba mkoani Kagera.

Msaidizi wa Mbunge Muhongo, Vaileth Peter amemkabidhi kijana Bina mahitaji hayo ikiwemo nauli leo Agosti 31, 2022 jimboni humo.

Kijana huyo alichelewa kuanza masomo ya kidato cha tano kutokana na kukosa mahitaji ya shule.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages