NEWS

Tuesday 16 August 2022

RC Mzee aomba wanahabari, viongozi wa dini Mara kushirikiana kuhamasisha sensaMkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee.

Na Shomari Binda, Musoma
------------------------------------

MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee, amewaomba viongozi wa dini, waandishi wa habari na viongozi wa mila kushirikiana katika kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi.

Akizungumza kwenye kikao na wadau hao wilayani Musoma jana, RC Mzee amesema uhamasishaji wa sensa hiyo unahitajika ili kufikia malengo ya Serikali.

“Nawaombeni nyote mkiwemo waandishi na vyombo vyenu tushirikiane katika kuhamasisha sensa itakayofanyika Agosti 23, 2022,” amesema Mzee.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ina nia njema ya kujua idadi ya wananchi wake na hali zao ili kuweza kuwahudumia.

Mkuu huyo wa mkoa amesema ushirikiano kutoka kwa wana-Mara katika maendeleo ataanza kuyaona kwenye uhamasishaji na ushiriki wa sensa hiyo.

Amesisitiza kuwa sensa hiyo itafanikiwa kwa asilimia 100 kama kutakuwa na ushirikiano wa pamoja.

Kwa upande wao, wadau hao wamesema wapo tayari kushirikiana katika kuhamasisha sensa hiyo.

Sheikh wa Mkoa wa Mara, Msabaha Kassim, amesema viongozi wa dini kupitia misikiti na makanisa wapo tayari kuhamasisha waumini wao kushiriki sensa hiyo kwa maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages