NEWS

Monday 8 August 2022

Timu ya Nyansisine FC yasepa na beberu la mbuzi baada ya kuichapa Bodaboda FC mashindano ya Sensa Cup



Nahodha wa Nyansisine FC, John Ogasi akiwkilisha timu yake kupokea zawadi ya beberu la mbuzi

Na Mara Online News
----------------------------

TIMU ya Soka ya Nyansisine FC imejinyakulia zawadi ya beberu la mbuzi lenye thamani ya shilingi 150,000 (pichani juu) baada ya kuibuka mshindi wa fainali ya mashindano ya Sensa Cup.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mizani Sirari wilayani Tarime jana Agosti 7, 2022, Nyansisine FC imeichapa Bodaboda FC bao 1-0.


Mchezaji wa Nyansisine FC akimiliki mpira uwanjani



Mashabiki wakifuatilia mechi hiyo ya fainali ya mashindano ya Sensa Cup

Nyansisine imekabidhiwa zawadi hiyo na mgeni rasmi katika mashindano hayo, Paul Siame ambaye ni Afisa Vipimo Kituo cha Sirari kilichopo mpakani na nchi ya Kenya.


Wachezaji na mashabiki wa Nyansisine FC wakishangilia ushindi

Bodaboda FC ambayo ni mshindi wa pili imezawadiwa soda kreti tatu, huku mshindi wa tatu Timu ya Mlimani FC ikipata soda kreti mbili.


Nahodha wa Bodaboda FC, Patrick Mosabi (kulia) akipokea zawati ya soda kreti tatu. Mwenyekoti nyeusi (kushoto) ni mwandaaji na mdhamini wa mashindano hayo, Boniface Samwel Peter.


Nahodha wa Mlimani FC, Amos Julius (kulia) akipokea zawadi ya soda kreti mbili

Aidha, mchezaji bora, mfungaji bora na goli kipa bora wa mashindano hayo wamezawadiwa viwango tofauti vya fedha taslimu.


Mwandaaji na mdhamini wa mashindano ya Sensa Cup, Boniface Samwel Peter (wa tatu waliokaa mbele) na viongozi wengine wakifuatilia mechi hiyo uwanjani.

Timu nyingine zilizoshiriki mashindano hayo ni Mizani FC, Gobaiya FC na Nyamaraga FC.

Mashindano hayo yalianza Julai 13, 2022 yakiwa yameandaliwa na kudhaminiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Ng’ereng’ere, Boniface Peter Samwel maarufu kwa jina la James Bwire.


Picha zote na Mara Online News

Boniface amesema aliamua kufanya hivyo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa wakati wa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages