NEWS

Wednesday 10 August 2022

TAKUKURU yamfikisha mahakamani mtumishi wa Rorya kwa uhujumu uchumi
Na Mara Online News
----------------------------

AFISA Mtendaji wa Kijiji cha Ruhu wilayani Rorya, Wambura Msimbete, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara kujibu shauri la uhujumu uchumi.

Shauri hilo namba 29/2022 limefunguliwa leo na Wakili wa Serikali, Yahaya Mwinyi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Wakili Mwinyi amesoma shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Yohana Myombo.

Ameiambia mahakama kwamba Msimbete alitenda kosa la ufujaji na ubadhirifu k/f 28 PCCA wa shilingi 2,285,150 alizokusanya kupitia mashine POS.

Mshitakiwa amekana kosa hilo na kuachiwa kwa dhamana hadi Septemba 6, 2022 kwa ajili ya kusikilizwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages