NEWS

Friday 12 August 2022

Wafugaji na wakulima Musoma Vijijini wako tayari kuhesabiwa
Na Mara Online News
----------------------------

WAFUGAJI na wakulima katika kijiji cha Nyasaungu kilichopo kata ya Ifulifu, jimbo la Musoma Vijijini, wameahidi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi kwa asilimia 100.

Wananchi hao wametoa ahadi hiyo juzi Jumatano, mbele ya Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo (pichani juu katikati), alipokwenda kuwaelimisha na kuwahamasisha kushiriki sensa hiyo.

“Sisi kama wafugaji na wakulima tuko tayari kuhesabiwa kwa sababu sensa itawezesha Serikali kujua idadi yetu na kutupatia huduma za kijamii kulingana na mahitaji yetu,” amesema mmoja wa wananchi hao.

Jana Alhamisi, Profesa Muhongo ameendelea na kampeni ya kuhamasisha ushiriki wa sensa hiyo katika kata za Bugwema na Bugoji.

Leo Ijumaa, Mbunge huyo aneendelea na kampeni hiyo katika kata za Nyambono na Etaro.

Kesho Jumamosi, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt Khalfani Haule anatarajiwa kuendesha kampeni hiyo katika kata ya Suguti.

Sensa ya Watu na Makazi itafanyika nchini kote siku ya Jumanne Agosti 23, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages