NEWS

Wednesday 14 September 2022

Ajali ya gari yakatisha maisha ya DED Igunga




MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya (DED) ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Latu (pichani) na madereva wawili wameripotiwa kufariki dunia katika ajali ya gari barabarani mkoani Mbeya.

Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mbeya, Juma Homera na Mwenyekiti wa Halmashauri yaa Wilaya ya Igunga, Lucas Bugota zimesema madereva waliofariki dunia ni wa gari la DED huyo na wa lori lililosababisha ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea leo Septemba 14, 2022 wakati Latu akitoka kuhudhuria kikao cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) jijini Mbeya, kwa mujibu wa taarifa hizo.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages