NEWS

Tuesday 25 October 2022

Mwenyekiti CCM Tarime apiga jeki Mbeza Sekondari wilayani Butiama

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho (wa pili kushoto), ametoa msaada wa shilingi milioni 2 kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Sekondari ya Mbeza wilayani Butiama, Mara.

Ngicho ambaye hivi karibuni alichaguliwa kwa kishindo kuendelea na wadhifa huo kwa mara ya pili - akiwatimulia vumbi washindani wake, amekabidhi msaada huo wakati wa Mahafali ya Pili ya Wahitimu wa Kidato cha Nne shuleni hapo leo Oktoba 25, 2022.


Katika mahafali hayo, Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Tarime amewakabidhi wahitimu hao vyeti na kuwahimiza kujiandaa vizuri kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye miihani wao ya kitaifa ujao. (Picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages