
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba (aliyevaa suti), leo Februari 11, 2026 amezindua na kukabidhi miundombinu ya utalii 21 iliyojengwa katika Hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha, Mikumi na Msitu wa Mazingira Asilia Kilombero.

Waziri Mkuu Mwigulu akizindua Uwanja wa Ndege Mtemere

Helikopta ikiwa katika Uwanja wa Ndege Mtemere
Ujenzi wa miundombinu ambayo Waziri Mkuu amezindua na kukabidhi umegharimu shilingi za Kitanzania billioni 114.62.
Lengo la kujengwa miundombinu hiyo ni kuongeza ubora wa vivutio vya utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kuimarisha usimamizi wa Maliasili na Utalii pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka hifadhi hizo, hususan kufungua shughuli za utalii ambazo zitasaidia kuleta ajira za moja kwa moja na sizizo za moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment