Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Gerald Ng'onga (wa pili kushoto) akisisitiza jambo katika kikao hicho Jumatano iliyopita. Wengine ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Chikoka (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Francis Namaumbo. (Picha na Sauti ya Mara)
Na Mwandishi Wetu, Rorya
------------------------------------------
WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya wamesimmishwa kazi wakidaiwa kijihusisha na manunuzi hewa ya vifaa ambavyo havitatumika kwenye ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Gerald Ng’ong’a aliwataja watumishi hao kuwa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Erick Mwita na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi, Mhandisi David Maganiko.
“Tumewapumzisha ili kupisha uchunguzi,” Ng’ong’a alisema muda mfupi baada ya kikao cha baraza la madiwani kuridhia uamuzi huo wilayani hapa, Jumatano iliyopita.
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho kumalizika, Ng’ong’a alisema watumishi hao wamehusika kufanya alichokiita madudu mengi hasiyovumilika kwani yanaisababishia halmashauri hiyo hasara ya mamilioni ya fedha.
“Yaani mtu unaanza kujenga msingi umeishanunua rangi. Halafu unanunua vifaa ambavyo havitatumika na kuna manunuzi hewa,” alisema Ng’ong’a ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Rabuor.
Alitolea mfano wa manunuzi ya ziada ya mifuko zaidi ya 700 na matofali 10,000 ambayo hayatatumika katika mradi wa ujenzi wa ukumbi wa halmashauri hiyo.
“Kuna vifaa vya ujenzi vya thamani ya shilingi milioni 64 kwa ajili ya kujenga ukumbi, lakini havitatumika na vimenunuliwa,” alisema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri hiyo.
Alisema manunuzi hewa yamehusisha mamia ya mifuko ya saruji na vigai, hivyo kusababisha baadhi ya miradi kukwama.
Aidha katika kikao hicho, watumishi wawili ambao ni wauguzi walishushiwa ‘rungu’ baada ya kikao cha baraza hilo kuridia kufutiwa utumishi wao kwa madai ya utoro kazini.
Chanzo: Sauti ya Mara
No comments:
Post a Comment