Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara halijaanza kutumika Kutokana na kukosa vitanda na magodoro licha ya bweni hilo kukamilika Agosti 2021 kwa gharama ya Sh120 milioni.
Bweni hilo lilijengwa kufuatia agizo alilolitoa Rais wa awamu ya tano hayati Dk.John Magufuli alipofanya ziara mkoani Mara Mwezi Septemba 2018 ambapo aliagiza wizara zinazohusika kutoa fedha kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.
Katika ziara hiyo hayati Dk Magufuli alitoa kiasi cha Sh20 milioni taslimu kwaajili ya ukarabati huo ikiwa ni njia mojwapo ya kumuenzi baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyesoma shuleni hapo miaka ya nyuma kwa elimu yake ya msingi.
Akizumguzma mjini hapa jana wakati akipokea msaada kutoka kwa wafanyakazi wa benki ya NMB matawi yote ya mkoa wa Mara, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwisenge B,Sigawa Thomas alisema kuwa kuwa vinahitajika vitanda 80 pamoja na magodoro 80 ili bweni hilo liweze kutumika.
"Hili bweni ni la wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum lina uwezo wa kulaza wanafunzi 80 halijaanza kutumika kutokana na kukosekana kwa vitanda na magodoro" alisema
Alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi mchanganyiko ina jumla ya wanafunzi 120 wenye mahitahi maalum ambao wote wanaishi bweni hivyo kutikana na bweni hilo kutokuanza kutumika wanafubzi hao wanalazimika kulala kwemye mabweni ya azmani ambapo mengine yamechakaa.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao, meneja wa NMB tawi la Tarime, Victorin Kiamrio alisema kuwa msada huo umetolewa na wafanyakazi hao ikiwa ni sehemu ya ya maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika.
Alifafanua kuwa wafanyakazi hao waliamua kuchanga fedha na kununua magodoro 80, luninga ya kisasa pamoja na king'amuzi vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh5.2 milioni kwaajili ya wanafunzi hao ambao ni wasioona, wenye mtindio wa ubongo, wenye ualbino pamoja na wenye ulemavu wa viungo.
"Tukiwa tunaadhimisha miaka 61 ya uhuru sote kwa umoja wetu tuliamua kufanya jambo japo kidogo kwaajili ya jamii ambapo tuliona ni vema tukalikumbuka kundi hili la watoto wenye mahitaji maalum ingawa tumetoa kidogo lakini tunafurahi kuwa tumeweza kuwafikia watoto hawa na hiki tulichokitoa kina mchango katika kufikia malengo yao ya kielimu" alisemaMeya wa Manispaa ya Musoma, William Gumbo aliwashukuru wafanyakazi hao kwa msaada huo ambao amesema kuwa umetolewa wakati muafaka.
"Tulikuwa tunawaza namna ya kupata vifaa vya humu ndani na nipende tu kutoa taarifa kuwa baada ya nyie kutoa taarifa juu ya kusudio lenu la kutapatia magodoro tayari kuna mdau naye ameahidi kutupatia vitanda vyote kwaajili ya bweni hili na muda wowote vitanda hivyo vitaletwa hivyo bweni letu litakuwa tayari kutumika mwakani "alisema.
No comments:
Post a Comment