NEWS

Thursday 15 December 2022

Ujenzi wa Chama: Chandi, Gachuma wazindua mashina matatu ya CCM Musoma Mjini



Na Mara Online News, Musoma
------------------------------------------------

MWENYEKITI mpya wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (wa pili kulia pichani juu) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa mkoa huo, Christopher Gachuma (kulia), wameanza rasmi kuendeleza ujenzi na uhamasishaji wa uhai wa chama hicho tawala kwa kuzindua mashina matatu katika Manispaa ya Musoma.

Mashina yaliyozinduliwa leo Desemba 15, 2022 ni Shina No: 03 Tawi la Mtakuja lililopo kata ya Mwisenge, Shina No: 03 Tawi la Mshikamano na Shina No: 09 lililopo eneo la Rwamlimi.

Chandi ametumia fursa hiyo pia kutoa mchango wa matofali 500 kusadia ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Rwamlimi. Viongozi wengine waliochangia ni Gachuma na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) - Viti Vitatu Tanzania Bara, Joyce Ryoba Mang'o ambao wametoa saruji mifuko kadhaa. 

Mwenyekiti Chandi (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chonchorio.

Baadaye Mwenyekiti Chandi amepokewa rasmi katika ofisi za CCM Mkoa wa Mara na kuongoza kikao chake cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kinachoendelea mjini Musoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages