NEWS

Saturday 31 December 2022

Papa mstaafu Benedict XVI afariki dunia mjini Vatican



PAPA wa zamani wa Kanisa Katoliki, Benedict XVI (pichani), amefariki dunia katika makazi yake Vatican, akiwa na umri wa miaka 95, karibu muongo mmoja baada ya kujiuzulu kwa sababu za kiafya.

Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki duniani kwa muda usiozidi miaka minane hadi mwaka 2013, akawa Papa wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII mwaka 1415.

Benedict aliishi miaka yake ya mwisho katika monasteri ya Mater Ecclesiae ndani ya kuta za Vatican.

Mrithi wake, Papa Francis alisema alikuwa anamtembelea huko mara kwa mara. Licha ya kwamba papa huyo wa zamani alikuwa mgonjwa kwa muda. Baraza Kuu lilisema hali ya afya yake imekuwa mbaya kwa sababu ya uzee.

Jumatano iliyopita, Papa Francis alitoa wito kwa hadhira ya mwisho ya mwaka huko Vatican kusali sala maalum kwa ajili ya Papa Emeritus Benedict, akisema alikuwa mgonjwa sana.

Benedict alizaliwa nchini Ujerumani na mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 78 akawa mmoja wa mapapa wakongwe kuwahi kuchaguliwa. BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages