NEWS

Monday 16 January 2023

Mjema hakuna kuchelewa, aanza kazi Idara ya Itikadi na Uenezi CCM TaifaKATIBU mpya wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi, Sophia Edward Mjema (pichani), amewasili na kuanza kazi ofisini kwake Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo Jumatatu Januari 16, 2022.

Akizungumza na watumishi na maafisa wa idara hiyo, Mjema amewataka kutekeleza majukumu yao kwa bidii, umoja, ubunifu na wakati wote kuhakikisha wanakuwa mfano bora katika kuendelea kujenga, kutunza na kulinda haiba nzuri ya CCM na Mwenyekiti wake wa Kitaifa, Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amesisitiza kuwa kazi kubwa iliyo mbele ni kuendelea kuyasema mazuri yanayofanyika kwa wananchi ili wayafahamu, kueleza uzuri wa CCM, kuwasikiliza wananchi kero au changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuendelea kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wa chama hicho tawala kupitia mafunzo.

“Kazi zote hizi hazipaswi kusubiri, tuanze sasa na tuendelee mbele,” Mjema amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages