NEWS

Sunday 1 January 2023

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, Chonchorio atua Jukwaa la Jambo TarimeNa Mwandishi Wetu, Tarime
------------------------------------------

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chonchorio (pichani) amejiunga rasmi na Jukwaa la Jambo Tarime na kuonesha ushirikiano wa kimaendeleo.

“Kwanza nimewapongeza na kuwaomba kuendelea kuwa na maono zaidi na mimi nitafanya sehemu yangu ikiwemo kuunganisha Jukwaa hili na wadau muhimu wa maendeleo,” Chonchorio ambaye ni marufu kama Chox aliwambia waandishi wa habari mara baada ya kupokewa rasmi kuwa mjumbe wa jukwaa hilo, katika hafla iliyofanyika kwenye hotel ya CMG mjini Tarime, juzi.

Chonchorio ambaye ni mwanasiasa kijana ambaye nyota yake imeonekana kung’ara katika sisasa za CCM wilayani Tarime kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, alishiriki pia kufanikisha changisho la shilingi laki saba la papo kwa hapo ili kumsaidia mmoja wa wajumbe wa jukwaa hilo anayeugua ili aweze kupata matibabu.

“Nimefurahi kuwa mwanafamilia wa Jukwaa la Jambo Tarime (Jambo Tarime) lenye wajumbe zaidi ya 200 ambao ni wazaliwa wa Tarime wanaoishi na kufanya kazi katika kona mbalimbali za nchi yetu,” alisema Chonchorio.

Akizungumzia ujio wa kiongozi huyo wa CCM ndani ya jukwa hilo ambalo halina itikadi za kisiasa, Kiongozi Mkuu wa Jambo Tarime, Daudi Magoko alisema hiyo ni ishara kwamba sasa watu wanaona uhumu wa shughuli za kijamii zinazofanywa na jukwa hilo lililoanzishwa mwaka 2014.

“Ni jambo kubwa na sisi tunajivunia kuwa jukwaa lenye watu ambao ni wanasiasa kutoka vyama mbalimbali, wasiokuwa na vyama, wanataaluma mbalimbali na wajasiriamali wadogo kwa wakubwa ambao tukikutano tunaongea lugha moja,” alisema Magoko.

Kila mwisho wa mwaka jukwaa hilo hukutanisha wajumbe wake kwenye sherehe zijijulikanyozo kama Jambo Tarime Day, tukio ambalo limekuwa likienda sambamba na utoaji wa misaada ya kijamii kwa wahitaji.

Mfano mwaka jana, jukwaa hilo lilipeleka misaada mbalimbali, ikiwemo TV, magodoro na sabuni kwa wafungwa na mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Tarime.

Miongoni mwa viongozi wengine waliohudhuria shere hizo hiyo ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Lucas Ngoto na Diwani wa Kata ya Nyanungu kupitia chama tawala - CCM, Tiboche Richard.

Chanzo: SAUTI YA MARA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages